Jumanne, 05 Rabi' al-thani 1446 | 2024/10/08
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Marekani Inatafuta Ushindi Madhubuti nchini Afghanistan
(Imetafsiriwa)

Na: Bilal Al-Muhajir – Wilayah Pakistan

Serikali ya Marekani, kupitia taasisi za kimataifa, hasa Umoja wa Mataifa, inalenga kupata ushindi madhubuti. Ni ushindi ambao haikuweza kuupata, licha ya zaidi ya miaka ishirini ya vita dhidi ya Uislamu na Mujahidina nchini Afghanistan. Utafutaji ushindi huu ulianza pale Marekani ilipoiruhusu Qatar kuwa mwenyeji wa vuguvugu la Taliban, na kufungua afisi kwa ajili ya vuguvugu hilo huko Doha mwaka 2013. Kupitia afisi hii, Marekani ilijihusisha kisiasa na harakati hiyo, na kusababisha duru kadhaa za mazungumzo yaliyohusisha Marekani na waamuzi, ukiwemo ujasusi wa Pakistan. Hatimaye, pande zote mbili zilikubali kukabidhi nchi kwa vuguvugu la Taliban, pamoja na kujiondoa kwa vikosi vya kijeshi vya Magharibi, lakini kwa mwendelezo wa “kipote cha washawishi wa wakuu serikalini” (Deep State) waaminifu kwa Marekani. Kipote hicho cha washawishi kilianzishwa kibaraka wa Marekani na Afghanistan ambaye Marekani ilimlimpandisha madarakani, Hamid Karzai, pamoja na waziri wake wa mambo ya nje Abdullah, Abdullah, ambaye alisimamia Baraza Kuu la Maridhiano ya Kitaifa la Afghanistan, pamoja na rais wa zamani Rabbani.

Ili kuhakikisha kwamba Marekani na dola za kikoloni za Magharibi zinahakikishiwa tena kuhusu mustakabali na uhalisia wa dola ya “kitaifa” ya Afghanistan, baada ya Mkataba wa Doha, walilazimisha masharti, mipango na miundo ya serikali, juu ya utawala wa harakati ya Taliban. Hii ilikuwa ni kuhakikisha kwamba dola ya harakati hiyo haitakuwa tofauti na dola nyengine za sasa katika Ulimwengu wa Kiislamu, ambazo zote zinatii Magharibi. Lengo muhimu zaidi lilikuwa ni kuzuia vuguvugu la Taliban kuunda serikali ya Kiislamu, au kutangaza dola ya Kiislamu inayotawala kipekee na kikamilifu kwa Quran Tukufu na Sunnah ya Mtume, njia ambayo maelfu ya Mujahidina wa Afghanistan waliuawa kishahidi kwa ajili yake.

Licha ya vuguvugu la Taliban kukubaliana na Makubaliano ya mwisho ya Doha kabla ya kuchukua madaraka mwaka 2021, na kukubali kuanzisha dola ya “kitaifa” ya Afghanistan, yenye sura ya Kiislamu, badala ya dola ya Kiislamu, Marekani haikukubali harakati na serikali yake kuingia katika klabu ya wakoloni wa Magharibi, kama wasaidizi wake wengine katika nchi mbalimbali za Kiislamu. Badala yake, Marekani iliendelea kuongeza masharti na maagizo kwa serikali hiyo. Katika kujibu, serikali ya harakati ya Taliban iliendelea kukubali na kutekeleza maagizo haya kama yalivyo. Kukubali na kutekeleza huku ni kwa kiwango ambacho Taliban hawakujiepusha tu kutabikisha hukmu za Shariah, bali pia walijiunga na muungano wa Magharibi katika vita vyake vya msalaba dhidi ya Uislamu. Serikali hiyo ilimuandama, kumfunga, na kumtesa yeyote anayetaka kutekelezwa kwa hukmu za Shariah, kinyume na madai yake ya hapo awali. Ilitaka hata wale wanaofanya kazi ya kusimamisha Khilafah kwa Njia ya Utume “watubu” na waache juhudi tukufu za kuhukumu kwa yale yote aliyoteremsha Mwenyezi Mungu (swt), kazi ya Mitume na Mitume madhubuti (as)! Kwa hivyo, harakati ya Taliban ilitumbukia katika mtego wa Magharibi, kama ilivyotajwa katika aya hii,

[وَلَنْ تَرْضَى عَنْكَ الْيَهُودُ وَلَا النَّصَارَى حَتَّى تَتَّبِعَ مِلَّتَهُمْ قُلْ إِنَّ هُدَى اللَّهِ هُوَ الْهُدَى وَلَئِنِ اتَّبَعْتَ أَهْوَاءَهُمْ بَعْدَ الَّذِي جَاءَكَ مِنَ الْعِلْمِ مَا لَكَ مِنَ اللَّهِ مِنْ وَلِيٍّ وَلَا نَصِيرٍ]

“Mayahudi hawawi radhi nawe, wala Wakristo, mpaka ufuate mila yao. Sema: Hakika uwongofu wa Mwenyezi Mungu ndio uwongofu. Na kama ukifuata matamanio yao baada ya ujuzi ulio kwisha kujia, hutapata mlinzi wala msaidizi kwa Mwenyezi Mungu.” [Surah al-Baqarah 2:120]. Kufuata njia ya maisha ya Mayahudi na Manaswara haikufungika tu katika imani. Inajumuisha itikadi na kanuni zote ambazo mikono yao imezitunga katika kumuasi Mwenyezi Mungu (saw), kama vile demokrasia, usekula, na fahamu za dola za kitaifa na kizalendo.

Sambamba na juhudi za Marekani na washirika wake za kufuatilia na kuandaa watoto wao nchini Afghanistan, raundi ya tatu ya mazungumzo ilianza mnamo Jumapili tarehe 30 Juni 2024 katika mji mkuu wa Qatar, Doha, kati ya maafisa wa Umoja wa Mataifa, wajumbe maalum nchini Afghanistan na wawakilishi wa serikali ya Taliban. Zaidi ya wajumbe ishirini, akiwemo Mwakilishi Maalum wa Marekani kwa Afghanistan, walikutana na ujumbe wa Taliban ukiongozwa na msemaji wake, Zabihullah Mujahid. Kama kawaida, Marekani na mashirika yake ya kikoloni, katika mazungumzo au mipango yoyote, huwasilisha ajenda ya juu juu kwa vyombo vya habari na matumizi ya umma, huku wakificha malengo mbalimbali ya kweli. Nyuma ya lengo lililotangazwa la Marekani la kujadili “haki za wanawake,” na dori ya mashirika ya kiraia nchini humo, kuna ajenda ya kuhakikisha dola ya harakati ya Taliban inafuata mipango iliyokubaliwa kati ya Marekani na harakati hiyo, ikiwemo kuigeuza jamii ya kihafidhina ya Afghanistan kuwa ya Kimagharibi, na kuwatumia vibaya wanawake wa Afghanistan katika soko la ajira. Hii ni sawia na kile kibaraka wa Marekani katika Bara Arabu, Salman, na mwanawe mzembe wanachofanya.

Ujinga wa kisiasa haukubaliki tena kutoka kwa vuguvugu, kundi, Mujahid, au mwanasiasa yeyote anayefanya kazi ndani ya Ummah. Hivi ndivyo hali ilivyo sasa kuliko wakati mwingine wowote, kwa vile kila mtu anafahamu ugumu wa njama za kisiasa, na hukmu madhubuti za Shariah, zinazoonya dhidi ya ushirikiano na makafiri, na kukataza kuwaunga mkono. Hakuna yeyote asiyejua ghilba za jamii ya kimataifa dhidi ya Uislamu na Waislamu, kwani haina nia yoyote njema kwetu. Kwa hivyo, hakuna udhuru kwa mtu yeyote!

Sheikh ambaye hivi sasa amefungwa kwenye jela za Mayahudi, mtetezi wa kuasisiwa Khilafah Rashida kwa Njia ya Utume, Sheikh Yusuf Makharza, amesema, الأعمال الصالحة التي تأتيها في الماضي هي رصيد لك في الآخرة وفي الدنيا، يثني الناس عليك بها ويحبونك لأجلها شريطة أن تبقى في المسار، فإذا كنت أمينا ثم صرت سارقا فإن النكير عليك يكون أعظم من النكير على من قضى عمره سارقا، وإذا كنت مجاهدا ثم صرت نصيرا للعدو تعينه على إخوتك فإياك أن تظن للحظة أن تاريخك أو تاريخ جماعتك يشفع لك، فكل نفس بما كسبت رهينة والتعاون مع العدو يسقط هيبتك ويذهب بكرامتك ويُحل عرضك ويُجرى عليك خلق الله، فالتوبة التوبة قبل فوات الأوان  “Matendo mema uliyoyafanya zamani ni mali yako Akhera na duniani. Watu watakusifu na kukupenda kwayo, mradi tu ubaki kwenye njia iliyo sawa. Ikiwa ulikuwa mwaminifu, kisha ukageuka kuwa mwizi, hukumu juu yako itakuwa kubwa zaidi kuliko ile ya mtu ambaye alitumia maisha yake yote kama mwizi. Iwapo ulikuwa Mujahid kisha ukawa mshirika wa maadui, ukawasaidia dhidi ya ndugu zako, ole wako usifikiri hata kidogo kwamba historia yako au ya harakati yako itakushufaiya. Kila nafsi imewekwa rehani kwa iliyo yachuma. Kushirikiana na adui kunaharibu utu wako, kunabatilisha heshima yako, na kukufanya udharauliwe na watu. Kwa hiyo, tubu kabla hujachelewa.”

Hivyo basi, viongozi walioghafilika wa harakati ya Taliban lazima warekebishe mwenendo wao. Ni lazima wakubali kile walichokikataa mwanzoni pale Hizb ut Tahrir ilipojitolea kusimamisha Khilafah kwa Njia ya Utume. Ikiwa uongozi wa vuguvugu hautarekebisha njia zake, wanachama waaminifu wa vuguvugu, ambao ni wengi, lazima warekebishe mikengeuko ya viongozi wao. Ni lazima wakabidhi mamlaka kwa wanasiasa waaminifu na wenye uwezo wa Hizb ut Tahrir. Hayo yatawapatia ridhaa ya wakaazi wa ardhini na mbinguni.

Mtume (saw) amesema,

«وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ لَتَأْمُرُنَّ بِالْمَعْرُوفِ وَلَتَنْهَوُنَّ عَنْ الْمُنْكَرِ أَوْ لَيُوشِكَنَّ اللَّهُ أَنْ يَبْعَثَ عَلَيْكُمْ عِقَابًا مِنْهُ ثُمَّ تَدْعُونَهُ فَلَا يُسْتَجَابُ لَكُمْ»

“Naapa kwa Yule ambaye nafsi yangu imo mkononi mwake, lazima muamrishe mema na lazima mukataze maovu, au Mwenyezi Mungu atakuteremshieni adhabu kutoka Kwake; kisha mtamuomba, naye hatakujibuni.” [Tirmidhi]

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu