Aqida ya Kiislamu Pekee ndiyo Msingi wa Dola, Katiba, na Sheria Lengo ni Uislamu Uingie Madarakani na sio Kutosheka na Muislamu Kuingia Madarakani
- Imepeperushwa katika Syria
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Uislamu umetuwajibisha kuifanya Aqiyah (itikadi) ya Kiislamu kuwa msingi wa dola, na wakati huo huo, msingi wa katiba na sheria. Yaani, chanzo pekee cha sheria. Haupaswi kuambatanishwa na vyanzo vyengine vya sheria, kama ilivyo katika katiba zilizotungwa na mwanadamu; baadhi yazo zinadai kwamba Uislamu ndio chanzo kikuu au chanzo msingi cha sheria, huku kiuhalisia wanaazima sheria ngeni kwetu kutoka Magharibi.