Nusra (Msaada) Inatafutwa Kutoka Kwa Nani?!
- Imepeperushwa katika Maswali ya Kimfumo
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Kutafuta Nusra (kuomba msaada) kunapaswa kufanywa kwa yule anayekubali Uislamu na kuuingia, na ambaye ni miongoni mwa watu wa nguvu na ulinzi, ili aweze kuinusuru dini na kusimamisha utawala kwa yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu. Masharti haya mawili lazima yatimie kwa mnayeitafuta Nusra kwake. Ikiwa hatakubali Uislamu na kuuingia, au si katika watu wa nguvu na ulinzi wenye uwezo wa kuleta mabadiliko, peke yake au pamoja na wengine, basi hatakuwa miongoni mwa watu wa Nusra



