Jumatatu, 04 Rabi' al-thani 1446 | 2024/10/07
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Je, Tunapaswa Kuzingatia Maneno Yako Mazuri au Matendo Yako Mabaya!

(Imetafsiriwa)

Habari:

Katika hotuba yake katika Programu ya Ufunguzi wa Wiki ya Mawlid al-Nabi Rais Erdoğan alisema, “Mtu pekee katika ulimwengu huu ambaye tunamuiga, tunafuata nyayo zake na ambaye tunajitolea maisha yetu kwake ni Mtume wetu wa Mwenyezi Mungu. Yeye ndiye kiongozi wetu na kipenzi chetu ambaye tutakufa kwa ajili yake. Mola wetu atujaalie tutembee katika nyayo za Mtume wa Mwenyezi Mungu, tujenge shakhsiya yetu kwa maisha yake, na tuwe na maadili mema ya kupigiwa mfano.” (Mashirika 14.09.2024)

Maoni:

Uovu mkubwa kabisa wanaoweza kuufanya watawala wanaochunga mambo ya watu, ni kuitawala jamii kwa mifumo inayotoka kwenye itikadi ya kisekula ambayo huwaweka watu mbali na Mola wao, ambayo huwafanya watumwa wa matamanio yao kwa udanganyifu wa uhuru na uliberali, na ambayo hutia utumwa kwa mja. Balaa kubwa zaidi kwa Waislamu ni dharau za watawala wanaotulazimishia masuluhisho ya fikra hizi za dhana potofu juu yetu. Rais Erdoğan ambaye ni gwiji wa kuongea kulingana na mapigo ya moyo, amejiwekea sifa ya kuzungumza kulingana na mazingira ya mchakato anaouingia. Kwa kuzingatia kanuni kwamba neno ni amana, ikiwa kiongozi pekee katika maisha yako ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na unadai kufuata nyayo zake, basi vitendo vyako vinapaswa kuthibitisha maneno haya mazuri.

Umakini na taqwa ya watawala wanaobeba mambo ya jamii katika maisha yao binafsi inahusiana na matendo yao na haihusu jamii. Hata hivyo, mifumo ya kikafiri na mawazo ya potofu ambayo yamewekwa kwa jamii itakuwa ni jukumu na lawama ya kila mtu binafsi, na hii ndiyo sehemu inayotuhusu. Katika muktadha huu, unaweza kuzungumza juu ya kufuata kiigizo cha Mtume wa Mwenyezi Mungu kadiri unavyotaka katika maisha yako binafsi, lakini maadamu kuna mfumo wa kidemokrasia wa kisekula wa ukafiri ambao kupitia kwayo unatawala jamii, matendo yako daima yatakinzana na maneno yako. Ubaya na harufu mbaya ya matendo yako itasumbua jamii daima. Tunategemea maneno ya watawala ambao matendo yao yatathibitisha maneno yao, ambao mwanzo watashikilia amana ya neno, ambao hawatausaliti Ummah na utukufu, na ambao wataifanya dini kuwa msingi wa utawala wao. Lakini Rais Erdoğan, kama nilivyotaja hapo juu, anaona ni siasa kuzungumza kulingana na mazingira na wakati, hivyo wakati mwingine anaionyesha Quran Tukufu kwenye viwanja vya uchaguzi. Nyakati nyingine, yeye huchochea umma kwa fasihi ya nchi na taifa. Wakati mwingine anaenda mbali zaidi na kuunadi usekula kwa watu katika sehemu mbalimbali za Jiografia ya Kiislamu kwa niaba ya Marekani. Demokrasia ni neno la kichawi ambalo kamwe halibanduki kwenye ulimi wake!

Bw. Erdoğan! Katika miaka yako 23 ya madaraka, ni hukmu ipi kati ya hukmu za Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) ambayo umeitekeleza ili useme kwamba unafuata nyayo zake na kwamba umemfanya kuwa kiongozi wako pekee? Je, udanganyifu, uhadaifu na upotoshaji wote uliofanya wakati wa utawala wako hautoshi! Kwa nini unasema mambo ambayo hukuyafanya, ambayo huwezi kuyafanya, kana kwamba umeyafanya, kana kwamba utayafanya, wakati huu ni mzigo mkubwa mbele ya Mwenyezi Mungu (swt)? Lau kweli ungefuata nyayo za Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), ungelikusanya jeshi zima na kukomesha dhulma hii huko Gaza ambayo imekumbwa na mauaji ya halaiki ambayo historia kamwe haijawahi kuyashuhudia mbele ya macho yako kwa muda wa mwaka mmoja. Hatutegemei sentensi za kupumbaza, bali tunategemea maneno ya watawala ambao ni kama watu wanaoyapamba matendo yao kwa hukmu za Uislamu.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) aziangamize nguvu za watawala Ruwaybidha, wanaoutesa Umma wa Kiislamu, na alete siku ambazo Makhalifa Rashid (walioongoka), ambao maneno na matendo yao ni kitu moja, watauongoza Ummah mara tu inawezekana.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Ahmet SAPA

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumatano, 25 Septemba 2024 15:11

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu