Jumanne, 05 Rabi' al-thani 1446 | 2024/10/08
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake

H.  14 Rabi' I 1446 Na: H 1446 / 024
M.  Jumanne, 17 Septemba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir Kinachapisha Barua ya Wazi kwa Majeshi ya Waislamu ili Kuikomboa Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina

(Imetafsiriwa)

Kama Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir, leo tumechapisha Barua ya Wazi kutoka kwa wanawake wa Umma huu mtukufu wa Kiislamu kwenda kwa ndugu, baba na wana wetu wanyoofu katika majeshi ya nchi za Kiislamu, tukiwataka wasimame kwenye wajibu wao wa Kiislamu wa kuwalinda Waislamu wa Palestina kutokana na umbile la mauaji la Kiyahudi, na kukomboa kila shubiri ya Ardhi hii Iliyobarikiwa kutoka katika makucha ya uvamizi huu wa mauaji ya halaiki. Barua hii itatafsiriwa katika lugha nyingi na kusambazwa kwa upana ndani ya jamii, kwenye mitandao ya kijamii na kwenye majukwaa mengine mbalimbali ya mtandaoni katika mabara yote.

Takriban watu 40,000 wameuwawa mjini Gaza katika kipindi cha miezi 10 iliyopita, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, huku serikali za ulimwengu, zikiwemo nchi za Waislamu zikitazama kama watazamaji pekee wa mauaji haya ya umwagaji damu, bila ya dhamira yoyote ya kisiasa ya kukomesha mauaji hayo. Hakika, tawala nyingi za ardhi za Kiislamu kwa miongo kadhaa zimeimarisha mkono wa uvamizi wa Kiyahudi kupitia mikataba yao ya amani, kuhalalisha mahusiano ya kidiplomasia, na ushirikiano wa kiuchumi na umbile hili la mauaji ya halaiki. Watawala na tawala hizi vibaraka zilizopandikizwa na nchi za Magharibi na zenye kutumikia Magharibi kama walinzi wa mstari wa mbele kwa umbile hili la mauaji na kuzuia harakati zozote dhidi yake. Wamewatelekeza Waislamu wanaodhulumiwa, wakaonyesha wazi wazi utiifu wao kwa umbile la Kiyahudi na wafadhili wake wa kikoloni wa Magharibi, na kuwafunga minyororo askari wao kwenye kambi zao huku Umma ukivuja damu.

Kwa hiyo ni juu ya mabega ya ndugu zetu wanyoofu na mashujaa katika majeshi ya Waislamu kuinuka na kukumbatia faradhi yao ya Kiislamu ya kuwa watetezi na wakombozi wa Waislamu, kwani wao ndio wenye uwezo wa kimada - vifaru, ndege silaha, askari - kutokomeza saratani hii ya uvamizi na kukomesha mauaji haya milele. Hakika, mafunzo yao yote, silaha na nguvu zao za kijeshi ni za nini ikiwa si kwa ajili ya kulinda Ummah wao na kukomboa ardhi zake? Zaidi ya hayo, usitishaji mapigano hautamaliza mauaji haya ya halaiki ya miongo saba na Nakba. Bali ni kukombolewa tu ardhi yote ya Palestina kutoka katika uvamizi huu wa mauaji wa kinyama ndio itakomesha mauaji, maumivu na mateso ya Waislamu wa Palestina. Na hili halitafikiwa bila ya kuhamasishwa kwa jeshi ambalo limejazwa na Iman.

Sisi kama wanawake wa Ummah huu wa Kiislamu tunawaambia ndugu zetu katika majeshi ya Waislamu, mpaka lini mtabakia kivulini na ilhali Ummah wenu unaangamizwa na ardhi ya Al Aqsa inanajisiwa?!! Je! Mtasema nini kwa Mola Mlezi (Rabb) wenu (swt) wakati Yeye (swt) atakapokuulizeni, وَمَا لَكُمْ لاَ تُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللّهِ وَالْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ الرِّجَالِ وَالنِّسَاء وَالْوِلْدَانِ الَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا أَخْرِجْنَا مِنْ هَـذِهِ الْقَرْيَةِ الظَّالِمِ أَهْلُهَا وَاجْعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ وَلِيًّا وَاجْعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ نَصِيرًا“Na mna nini msipigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu na ya wale wanao onewa, wanaume na wanawake na watoto, ambao husema: Mola Mlezi wetu! Tutoe katika mji huu ambao watu wake ni madhaalimu, na tujaalie tuwe na mlinzi anaye toka kwako, na tujaalie tuwe na wa kutunusuru anaye toka kwako.” [An-Nisaa: 75]? Tunakuombeni muinuke na kuvipindua viti vya watawala hawa waoga wasaliti wa Waislamu ambao wamelichafua jina lenu, na mufutilie mbali mipaka hii batili ya kizalendo iliyowekewa na wakoloni kati ya ardhi zetu, na muandamane hadi Al Quds kwa ulinzi wa mama zenu na watoto wenu wa Palestina. Na mutoe Nusrah yenu (msaada wa kimada) kwa ajili ya kusimamisha uongozi wa Kiislamu na Mfumo wa Mwenyezi Mungu (swt) - Khilafah kwa njia ya Utume ambayo ni mchungaji, mlinzi na ngao ya Waislamu. Ni dola hii pekee ndiyo itakayokuhamasisheni kutimiza dori yenu ya kweli kama watetezi, wakombozi na walinzi wa Umma na Dini yenu kama Mwenyezi Mungu (swt) anavyoamrisha, kukufanyeni mashujaa wa Waislamu na kuleta heshima kwa jina lenu. Nyinyi ni warithi wa viongozi na makamanda watukufu wa Uislamu kama vile Salahuddin Ayubi (RH), Muhammad ibn Qasim (RH), na Muhammad al Fatih (RH). Kwa hivyo kumbatieni urithi wao wa kupata ushindi mkubwa kwa Dini yenu, pamoja na ukombozi wa Al Aqsa. Kwa hivyo musichelewe! Wakati wa kuchukua hatua ni sasa!

Kusoma Barua Hiyo Bonyeza Hapa

Kutazama Video Bonyeza Hapa

 

Kitengo cha Wanawake

katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

 

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
Address & Website
Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizbuttahrir.today
Fax: Telefax
E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu